Thursday, 31 October 2013

Kenya yashambulia kambi ya al Shabab Somalia

Ndege za kijeshi za Kenya zimeshambulia ngome za kundi la al Shabab ndani ya ardhi ya Somalia. Shambulizi hilo limetajwa kuwa linahusiana na hujuma ya kigaidi iliyofanywa na al Shabab mjini Nairobi zaidi ya mwezi mmoja uliopita na kuua watu karibu 70.

Tusikubali kuivunja Jumuia ya Afrika Mashariki

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa sasa inapitia katika kipindi kigumu baada ya nchi za Rwanda, Uganda na Kenya kuanzisha ushirikiano wa peke yao huku zikizitenga Tanzania na Burundi.

Mabadiliko makubwa mitihani ya sekondari

Dar es Salaam. Zikiwa zimebaki siku tatu kwa wanafunzi wa kidato cha nne kuanza mtihani wa kumaliza ngazi hiyo ya elimu, Serikali imepunguza alama za ufaulu kwa mtihani huo pamoja na ule wa Kidato cha Sita.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa laweza kuidhinisha kuongeza askari wa AMISOM


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana Jumatano (tarehe 30 Oktoba) ili kuzingatia kuongeza nyenzo na askari kwa ajili ya Misheni ya Umoja wa Afrika kwa Somalia (AMISOM), ambalo wanadiplomasia wanasema ni mu