Ndege za kijeshi za Kenya zimeshambulia ngome za kundi la al
Shabab ndani ya ardhi ya Somalia. Shambulizi hilo limetajwa kuwa
linahusiana na hujuma ya kigaidi iliyofanywa na al Shabab mjini Nairobi
zaidi ya mwezi mmoja uliopita na kuua watu karibu 70.
Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) limetangaza kuwa ndege zake za kijeshi
zimeshambulia kambi ya mafunzo iliyokuwa ikitumiwa na wanachama wa al
Shabab ndani ya Somalia. Shambulizi hilo linafuatia lile la Jumatatu
iliyopita ambapo viongozi wawili wa kundi hilo waliuawa.
Msemaji wa jeshi la Kenya Kanali Cyrus Oguna amesema kuwa shambulizi
la jana ni sehemu ya operesheni kubwa zaidi ya kikosi cha jeshi la Umoja
wa Afrika AMISOM ambayo inalenga kambi za mafunzo za kundi la al
Shabab. Oguna amesema watu waliofanya mashambulizi dhidi ya jumba la
maduka la Westgate jijini Nairobi tarehe 21 Septemba walipata mafunzo
katika kambi hiyo.
Kambi hiyo ilikuwa na wapiganaji 300 wa al Shabab na jeshi la Kenya linasema kuwa wengi wao wameuawa au kujeruhiwa.
Kanali Cyrus Oguna amesisitiza kuwa mashambulizi dhidi ya ngome za wapiganaji wa al Shabab yataendelea.
Air01/11/13 Araqchi: Urutubishaji
No comments:
Post a Comment