Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana Jumatano (tarehe 30 Oktoba) ili kuzingatia kuongeza nyenzo na askari kwa ajili ya Misheni ya Umoja wa Afrika kwa Somalia (AMISOM), ambalo wanadiplomasia wanasema ni mu
Baraza linatarajiwa kupiga kura kuunga mkono ongezeko la askari
4,000, na kuweka kikomo cha wafanyakazi wa AMISOM nchini Somalia kufikia
22,000, AFP iliarifu.
Naibu Katibu Mkuu wa UN Jan Eliasson aliliambia baraza kwamba AMISOM
imepata mafanikio makubwa dhidi ya al-Shabaab, lakini hivi karibuni
juhudi zao "zimepungua" kwa sababu ya kukosa idadi kubwa ya askari.
"[Al-Shabaab] inatembea na inawapatia mafunzo na kuwaajiri idadi
kubwa ya vijana waliovunjika moyo na kukosa ajira," Eliasson aliliambia
baraza.
Alithibitisha wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na Umoja wa Afrika wa "ongezeko kubwa la muda" kwa idadi ya askari wa AMISOM.
Umoja wa Afrika umesema unahitaji nyongeza ya askari wa miguu 25,000 na askari 1,800 wa kusaidia.
Ban alisema kuwa katika taarifa ya karibuni kwa Baraza la Usalama
kwamba kulikuwa na haja ya dharura ya kuimarisha AMISOM ili kuelekea
kusini ya Somalia ili "kuwanyima al-Shabaab fursa ya kuongeza rasilimali
na kuandikisha na kuwapa mafunzo watu kwa nguvu".
himu katika kuondosha tishio lililopo la al-Shabaab.
No comments:
Post a Comment