Kiongozi wa zamani wa waasi katika Jamhuri ya
kidemokrasia ya Bosco Ntagandaa amefikishwa katika mahakama ya
kimataifa ya makosa ya jinai ICC huko The Hague
.Mwendesha mkuu wa mashitaka ICC,Fatou Bensouda amesema kuwa Ntaganda aliamuru watu kuwaua na kuwabaka waathiriwa wa vita.
Bosco Ntaganda -- anayefahamika sana Nchini Congo kwa jina Terminator yuko mahakamani kama mshukiwa wa kwanza kuwahi kujisalimisha mwenyewe.
Alijisalimisha katika ubalozi wa Marekani Nchini Rwanda mwaka jana.
Bwana Ntaganda ambaye ni mshukiwa aliyekuwa akisakwa zaidi na ICC anatuhumiwa kutekeleza makosa 18 ikiwemo kuwatumia wasichana kama wafungwa wa ngono.
Majaji katika kesi hiyo wataamua kama Ntaganda ana kesi ya kujibu au la.
No comments:
Post a Comment