Taifa la Tanzania ni taifa ambalo watu wengi wan je wanaamini
kuwa watu wake ni wenye huruma sana na pia wanabusara kiasi kwamba hawawezi
kuvumilia kuona ndugu zao wanapote lakini mbona jambo hili au dhana hii
inatoweka hasa pale ambapo suala la uchangiaji damu inapoletwa miongoni mwetu
ikituhitaji tufanye hivyo tunakwepa?
Changia damu kama tendo la huruma kwa ndugu zako
usiowafahamu na kuamini kuwa damu hiyo itatumika siku moja kwa mwanao pindi
utokapo toweka .
Mzee huyu ni moja ya watanzania wenye huruma ambao kila
mwezi hujitolea kutoa damu akiamini anamuokoa mwanae au ndugu yake ambaye
asiongependa apotee wakati nafasi ya msaada upo wazi kwake.
Ungana na mamia ya
watanzania kuchangia damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya mamia ya watanzania
inayopotea wakati kuna uwezekano wa kuwaokoa.
No comments:
Post a Comment