Watu wawili wamekamatwa baada ya kupatikana wakiwa na
maguruneti mawili nyumbani mwao wakati polisi wakiendelea na msako
mkali mtaani Easteligh nchini Kenya.
Wawili hao, Mume na mkewe walikuwa nyumbani wakati polisi walipopata habari kuwahusu na vifaa walivyomiliki.
Polisi wamekuwa wakifanya msako katika mtaa huo wa Easteligh tangu mashambulizi ya maguruneti kuwaua watu 6 Jumatatu usiku na kuwajeruhi wengine 30.
Mkuu wa polisi alisema kuwa wawili hao walikamatwa pamoja na watu wengine 400 katika eneo hilo huku msako wa polisi ukiendelea.
Polisi wanasema kuwa wanawahoji wawili hao kuona ikiwa wanaweza kupata taarifa zaidi
Takriban watu 657 walikamatwa na polisi Jumatatu usiku mtaani Eastleigh, baada ya shambulizi la kigaidi dhidi ya mkahawa kuwaua watu sita.
No comments:
Post a Comment