Tuesday, 3 December 2013

Marais wa nchi wanacham wa EAC wasaini mkataba wa kuanza mchakato wa kuwa na sarafu moja

















Wakuu wa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, wamesaini mkataba wa kuanza mchakato wa kuwa na sarafu moja itakayotumika katika nchi zote wanchama wa jumuiya hiyo.

Sherehe za kutia saini mkataba huo zilifanyika jana jumamosi jijini Kampala nchini Uganda ambako viongozi wa Mataifa matano wanachama walikutana.

Marais wa Mataifa ya EAC, Yoweri Mseveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya, Jakaya Kikwete wa Tanzania, Paul Kagame wa Rwanda na Pierre Nkuruzinza wa Burundi walihudhuria kikao cha 15 cha umoja huo ambacho kilichofikia maamuzi hayo jana jumamosi.
Akizungumza katika kikao hicho, Katibu wa EAC Richard Sezibera alisema hatua hiyo inathibitishauanzishwaji wa matumizi ya sarafu moja mara mchakato wa maandalizi utakapokamilika na hii ni hatua mojawapo ya kuhakikisha nchi za EAC zinafikia azimio la kuwa na shirikisho la kisiasa ambalo ni hatua ya juu kabisa.
Umoja wa sarafu ni miongoni mwa malengo makuu manne yaliyoainishwa katika mkataba wa EAC, mengine ni soko la pamoja na umoja wa forodha ambayo tayari mikataba yake imeanza kutekelezwa.
Katika kikao hicho cha Kampala Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alichukua uenyekiti wa jumuiya hiyo kutoka kwa Rais wa Rwanda, Paul Kagame.
Aidha viongozi hao walikubaliana watakuwa wanashauriana mara kwa mara kuhusu maswala muhimu yanayohusu jumuiya nzima ya EAC.

No comments:

Post a Comment