Jenerali Amadou Haya Sanogo kiongozi wa wafanya mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Machi 2012 nchini Mali, leo ametiwa mbaroni.
Taarifa zinasema kuwa, makumi ya wanajeshi wa Mali mapema leo wamevamia nyumba ya Jenerali Sanogo katikati mwa Bamako, mji mkuu wa nchi hiyo na kumtia mbaroni kiongozi huyo wa mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika mwaka jana. Afisa mmoja mwandamizi wa jeshi la Mali amesema kuwa, Jenerali Sanogo ametiwa mbaroni baada ya kukataa amri ya mahakama ya kuhudhuria mahakamani.
Sanogo akiwa pamoja na maafisa wengine wa ngazi za juu wa jeshi la Mali, aliongoza mapinduzi ya kijeshi mwezi Machi mwaka 2012 na kumuondoa madarakani rais wa wakati huo wa Mali Amadou Toumani Toure ambaye aliingia madarakani baada ya kuchaguliwa na wananchi.

No comments:
Post a Comment