Polisi nchini Kenya wamesema kua hali ya utulivu
imerejea katika kijiji kilichokuwa kimezingirwa na wavamizi kutoka jamii
hasimu katika jimbo la Turkana Kaskazini Magharibi mwa Kenya.
Washambulizi walivamia kijiji chaKlooigon kilichokuwa na karibui wakaazi 900 ambao walizuia kuondoka.
Msemaji wa Polisi alisema kuwa hali ilitulizwa baada ya viongozi wa jamii hizo mbili ambazo huzozania mali asili mara kwa mara kuingilia kati na kuwashawishi wavamizi kuondoka kutoka eneo hilo.
Duru zinasema kuwa hakuna mtu alijeruhiwa na kuwa polisi wangali wanaondoa vizuizi vilivyo kua vimewekwa barabarani ili kuwazuia kuingia katika kijiji hicho.
Maafisa wa utawala waliweka sheria ya kutotembea usiku mnao siku ya Jumamosi baada ya wavamizi kuingia Lorogon.
Shirika la msalaba mwekundu linakadiria kuwa karibia watu 600 hadi 900 walikuwa katika kijiji hicho, kilichokuwa kimezingirwa na wavamizi 150.
Kwa mujibu wa shirika hilo, hali ilianza kutokota mwezi Novemba tarehe 18 baada ya watu wawili wa jamii ya Pokot kuuawa,mauaji ambayo waturkana walidaiwa kuyatekeleza.
Katika hali ya kulipiza kisasi, watu wa jamii ya Pokot nao wakaamua kuwashambulia waturkana
Jamii hizo mbili zimekuwa zikizozana hasa kuhusu malisho ya mifugo wao.
No comments:
Post a Comment