Mahakama ya Katiba ya Zimbabwe imefuta sheria ya adhabu dhidi ya wanaomdhalilisha Rais wa nchi hiyo.
Awali sheria ya Zimbabwe ilikuwa ikiwazuia raia kukosoa na kuchunguza utendaji wa Rais Robert Mugabe au kumvunjia heshima,
na mtu yeyote aliyekiuka sheria hiyo alichukuliwa hatua za kisheria. Sheria hiyo pia ilipiga marufuku kuchapisha habari za uongo zinazodhoofisha uwezo wa Rais wa nchi.
Kwa msingi huo katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita makumi ya watu wamekamatwa na kuswekwa jela kwa kosa eti la kumkosoa Rais wa Zimbabwe au kuhoji utendaji wake katika nyanja mbalimbali. Wanaharakati wa jumuiya zisizo za serikali wanasema kuwa, chini ya sheria hiyo zaidi ya watu 60 wamekamatwa na kufungwa jela katika miaka mitatu iliyopita. Miongoni mwa watu mashuhuri waliokumbwa na fagio la chuma la sheria hiyo ni kiongozi wa vijana wa chama cha upinzani cha MDC Solomon Madzore. Katika mojawapo na mikutano ya wapinzani wa serikali Madzore alimfananisha Rais Robert Mugabe na farasi aliyechoka. Mugabe anayeingoza Zimbabwe tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1980 ana umri wa miaka 89.
Mahakama ya Katiba ya Zimbabwe imesema kuwa sheria hiyo inakiuka uhuru wa kujieleza na inapuuza vigezo vya katiba mpya kuhusu udharura wa kuheshimiwa haki za binadamu na uhuru wa kijamii.
Katiba mpya ya Zimabwe ilipasishwa mwezi Machi mwaka huu baada ya malumbano na mvutano mkali baina ya wawakilishi wa chama cha Zanu-PF cha Rais Robert Mugabe na wale wa chama cha Harakati ya Mabadiliko ya Kidemokrasia (MDC). Kupasishwa kwa katiba hiyo ni hatua muhimu katika njia ya kuelekea kwenye demokrasia nchini Zimbabwe.
Katiba mpya ya Zimbabwe imewapa madaraka makubwa zaidi wabunge na kubana kipindi cha rais katika vipindi viwili vya miaka mitano mitano. Hata hivyo katiba hiyo haikuleta mabadiliko makubwa katika uongozi wa Zimbabwe, kwani Mugabe ambaye ameingoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 33, alishinda tena katika uchaguzi uliofanyika tarehe 31 Julai mwaka huu.
Alaa kulli haal, uamuzi wa Mahakama ya Katiba ya Zimbabwe wa kufuta sheria hiyo umekuwa na taathira nzuri katika hali ya kisiasa ya nchi hiyo na imepongezwa na watu wengi. Vilevile suala hilo linaweza kuwa na faida kwa chama tawala cha Zanu-PF hususan baada ya wasimamizi wa Ulaya kutilia shaka matokeo ya uchaguzi wa Rais ambayo pia yamepingwa na wafuasi wa kambi ya upinzani.
imetolewa:idhaa ya kiswahili ya radio tehran

No comments:
Post a Comment