Wednesday, 27 November 2013

Berlusconi ajadiliwa kutimuliwa














Bunge la seneti nchini Italia linajadili hoja iwapo Waziri Mkuu mstaafu wa Italia Silvio Berlusconi atimuliwe au la kutokana na kupatikana na hatia ya kukwepa kulipa kodi.
Wachambuzi wanasema hoja ya kumtimua inatarajiwa

 kuungwa mkono na maseneta wengi.
Kwa upande Berlusconi amewaambia wafuasi wake kuwa leo ni siku ya maombolezo katika demokrasia na kwamba kura hiyo ya bunge la seneti inaonyesha chuki binafsi ya wale wa upande wa kushoto.
Berlusconi alijiondoa siku ya jumanne katika chama cha Forza Italia ambacho kipo ndani ya serikali ya mseto inayotawala nchi hiyo, hata hivyo serikali iliepuka kura ya kutokuwa na imani na kufanikiwa kupitisha bajeti.
Mjadala katika bunge la seneti umekuwa mkali ambapo maseneta kutoka pande zinazopingana wamekuwa wakitupiana maneno makali.
Manuela Ripetti kutoka chama cha Berlusconi cha Forza Italia alisikika akipaza sauti "Tunajua nia yenu ni kumwondoa Silvio Berlusconi".
Berlusconi ambaye ametawala katika siasa kwa miongo miwili nchini Italia amewaomba maseneta kusogeza mbele kura hiyo ya kumwondoa kwa madai kwamba anao ushahidi unaothibitisha kuwa hajafanya kosa la kukwepa kodi.

No comments:

Post a Comment