Tuesday, 26 November 2013

Jaji Mkuu aagiza kesi ya Mramba, wenzake iharakishwe
















Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman, ameagiza kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia Serikali hasara

 ya Sh11.7bilioni inayowakabili mawaziri wawili wa zamani na katibu mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha, imalizwe haraka.
Mawaziri hao ni Basil Mramba na Daniel Yona na katibu Grey Mgonja, ambao kesi yao iko  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wanatuhumiwa  kutumia vibaya madaraka yao kwa kuisamehe kodi, Kampuni ya Ukaguzi wa Madini ya Alex Stewart, kinyume cha sheria.
Hayo yalibanishwa jana na Hakimu Mkazi  Alphan  Isaya, wakati akiahirisha kesi hiyo.Jana ilikuwa siku ya kuendelea kusikiliza utetezi wa washtakiwa hao, lakini mshtakiwa Yona hakuwepo mahakamani.
Awali, Wakili wa Serikali, Oswald Tibabyekomya, alisema kesi hiyo ilipangwa kuendelea kusikilizwa.
Hata hivyo Wakili wa utetezi, Eliasa Msuya, aliieleza mahakama  kuwa Yona hakuwepo mahakamani na kwamba  yuko India, kwa matibabu na kwamba ana kibali cha mahakama, kilichotolewa Oktoba 8 mwaka huu.
Kutokana na maelezo hayo ya wakili wa utetezi, Wakili wa Serikali, Tibabyekomya,  aliiomba mahakama, upande wa utetezi ueleze ni lini atakuwepo.

No comments:

Post a Comment