Friday, 1 November 2013

Wananchi wa kenya wapinga adhabu ndogo dhidi ya wabakaji

Mamia ya wanawake wa Kenya wameandamana wakipinga adhabu ya kufyeka majani katika ua wa kituo cha polisi waliyopatiwa wabakaji wa mwanafunzi.

 Maandamano hayo yaliyofanyika katika mji mkuu wa Kenya Nairobi yamewashirikisha mamia ya akina mama ambao wanalalamikia adhabu ya kukata majani katika uwanja wa uwanja wa kituo cha polisi waliyopatiwa genge lililombaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16. Maandamano hayo yaliishia katika vituo vya polisi jijini Nairobi kwa kukabidhi majina zaidi ya watu  milioni moja yanayotoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kiadilifu dhidi ya kundi lililombaka msichana wa miaka 16 na kumfanyia vitendo vya kinyama. Taarifa zaidi zinasema kwamba, msichana huyo wa miaka 16 alipigwa vibaya na kisha kubakwa na wanaume sita wakati alipokuwa akitoka katika mazishi ya babu yake magharibi mwa Kenya Juni mwaka huu.
Baada ya kubakwa msichana huyo alitupwa katika mtaro wa maji machafu. Kwa sasa binti huyo anatembelea baiskeli ya magurudumu kutokana na madhara ya mgongo aliyoyapa ambayo inasadikiwa yalitokana na kutupwa mtaroni au kupigwa. Polisi ya Kenya imeahidi kufanya uchunguzi kuhusiana na kesi hiyo.

No comments:

Post a Comment